TATIZO LA VIFARANGA KUGANDIANA CHOO KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA
Katika malezi ya
vifaranga kumekuwa na tatizo sugu ambalo kwa bahati mbaya wafugaji wengi
hawalijui na limekuwa jikiwatesa sana. Vifaranga wadogo walio chini ya umri wa
wiki moja wamekuwa na katizo la kugandia kwa kinyesi nje ya njia zao za haja
yaani kwenye kale ka tundu kakutolea kinyesi. Wakati mwingine huziba kabisa
njia ya choo na kumsababishia kibo kifaranga lakini hata asipokufa hukosa raha
na mwishowe kuwa na ukuwaji usiokuwa mzuri.
Kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa Zaidi ya 50% ya vifaranga wanaopata tatizo hilo hufa kama wasipopata huduma inayostahili. Mara nyingi unaweza kushangaa vifaranga wako wanakosa raha, wanakufa, nk. Lakini ukimchunguza utamkuta na uchafu kwenye njia zake za kutolea haja kubwa nap engine huwa ameziba kabisa.
Tatizo hili husababishwa na kuwapa chakula kingi vifaranga na kuwapa maji kidogo au wasipate kabisa. Kifaranga anapozaliwa kama kiumbe mwingine huwa hajawa imala katika maumbo yake na mfumo wake wa mmengenyo hivyo unapompa chakula bila maji ya kutosha ni kwamba hata upataji kake wa choo utakuwa wa tabu.
Kuepuka hili tatizo unapaswa kuanzia siku moja hadi 5 kuhakikisha vifaranga wako wanapata maji mengi na chakula cha wastani ili kumuwezesha njia zake za mmengenyo kukaa sawa na kutoathirika na vitu vikavu na vigum. Ili kuliwezesha hili nawashauri wafugaji wenzagu mhakikishe vifaranga wenu mnawapa maji ya kutosha ili kuepukana na kadhia hiyo. Pia natoa angalizo na fundisho kuwa, vifarnga wadogo hawawezi kujishughurisha sana kutafuta chakula/maji yalipo badala yake yake kinavhokuwa mbele yake anakula na kama hakuna kitu bas, sasa akikuta chakula bila maji then tatizo kinaanzia hapo.
Jinsi ya kuahudumia wakioathirika ni kuwasafisha kwa kutumia maji ya uvuguvugu au kito chochote mithiri yake ili kuhakikisha unauondoa uchafu ule bila ya kumuumiza na njia yake ya haja ibaki safi. Wakati huo huo uanapendeza ukiwa unampatia antibacterial ili kumuepusha na madhara Zaidi ya yapo na pia inashauriwa kuwa unampaka mafuta ya mgando asili ya jelly kwaajili ya kumlainisha njia yake ya haja ili asiumie Zaidi.
Kwa mafundisho kama haya na mengine usikose ku like na kuwa unafitia mara kwa mara kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa ajili ya kuyapata kiurahisi.
Utatupata
kwa kupitia
https://web.facebook.com/www.bbp.co.tz/…
KARIBUNI SANA

0 comments:
Post a Comment