Our social:

Friday, October 28, 2016

UTAJUAJE UFUGE KUKU WA AINA GANI?


Kumekuwa na bleed/ makabila mbali mbali ya aina za kuku haswa hawa machotara hawa akina kari, kroiler, Malawi, sasso, izrael nk. Kitu ambacho humpa mfugaji wakati mgumu wa kujua ni kuku wa aina gani uwafuge kwani mara nyingi wamekuwa wakikutana na wauzaji ambao kila mmoja anajinadi kuwa bidhaa yake yeye ndo best. Katika kuchagua mbegu ipi ufuge kuna hoja nyingi za kuzingatia ikiwa ni pamoja na uwezo wa kupambana na magonjwa, matunzo, kasi ya ukuaji, nyama tamu, nyama nyingi, mayai mengi nk.
Ukijaribu kuzichunguza hizi mbegu zote utagundua kuwa kila mbegu kila mmoja ana uzuri wake, ana ubaya wake na sababu nyingi ni zinafanana katika sifa nyingi isipokuwa sifa kuu 2 ambazo zinafanana pia kwa kiasi flani lakini zinakuwa na utofauti japo ni kidogo lakini inakuwa na maana kubwa katika mradi wa kuku.
Ili ujue ni mbegu gani inakuhusu hasa ni malengo yako tu ndo yatakusaidia kulitambua hilo ambavyo malengo yenyewe yamegawanyika mara mbili kuu. Je unahitaji kwa ajili ya kuuza kuku wa kitoweo au kwa ajili ya kuzalisha/mayai/kutotolesha. Kama unahitaji kuuza kuku inabidi ununue kuku wenye nyama na watam ndo ambao hawatakusumbua sokoni, lakini kama unataka kwa ajili ya mayai / kutotolesha kwa wingi lazma uchague anayetaga Zaidi. 


Unachopaswa kujua ni kwamba hakuna mwenye sifa zote at best level, lazma uamue kuchagua moja kama ni mayai au nyama. Na ieleweke pia si kwamba wa mayai hawana nyama au hawaliki, na wa nyama hawatagi, nop, ni kwamba wanavyo bali unaangalia what is best. Kwa maana utakuwa unapata hata kingine lakini sio kama wa mbegu nyingine.


Kwenye mradi wa kuku pia lazma upange na kuchagua kama ilivyo katika miradi mingine na mipango yoyote. Lazma ufike sehemu uamue kimoja kwamba wewe unahitaji nini haswa then mambo mengine yawe nyongeza. Hupaswi kuanza kufuga bila kujua malengo yako ni yapi ili ujue unajikita wapi kwenye kupanga na kuchagua kwa maana uchukue mbegu ipi.


Usifanye kitu kwa fasheni kwamba unafuga aina flani kwakuwa imepigiwa chapuo sana au flani/ rafiki yako kafuga, hapana, jitafakari wapi panakufaa then ndo upafate na sio kufata mkumbo. Ufugaji ni mzuri na unalipa tena sana lakini sio ufugaji wa kukurupuka, jitafakari ndo uamue na utende.
Kwa mafundisho kama haya na mengine usikose ku like na kuwa unafitia mara kwa mara kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa ajili ya kuyapata kiurahisi. Utaupata kwa kupitia
https://www.facebook.com/www.bbp.co.tz/…
KARIBUNI SANA






0 comments:

Post a Comment