ULEAJI WA VIFARANGA
Watu wengi wamekuwa wakifeli na kukata tamaa kwa kukosa
uwezo na uelwa sahihi wa namna ya kulea vifaranga kwa maanamtu anachukua bila
ABCD… za vifaranga. Ili ufanikiwe kuwakuza vifaranga sio kazi ngumu wala sio
kazi nyepesi, ni vile tu kuwajulia jinsi ya kwenda nao vizuri. Malezi ya Vifaranga yanaanzia mbali sana tofauti na wengi wanavyofikiria, watu
wanachukulia malezi ya vifaranga ni kuanzia vifaranga wakitotolewa, kitu
ambacho sio kweli, malezi ya vifaranga yanaanzia kwa mama mtagaji. Ili
ufanikiwe kuwalea vifaranga lazma uzingatie yafuatayo;
1. Mama asiye na magonjwa, watu wengi hawajui lakini ndo
ukweli kwani kunayo baadhi ya magonjwa yanaambukuzwa toka kwa mama mtagaji wa
yai, hata kama utatumia njia gani za kutotolesha lakini kama wale watagaji wana
magonjwa basi ni rahisi sana kuwaathiri mpaka vifaranga watakaotokana nao.
Mfano kama mama ana mafua sugu ni vigum sana kwa kifaranga chake kuishi .
2. Maandalizi kabla ya kupokea vifaranga, kabla hujaingiza
vifaranga kwenye eneo lako unalotegemea kuwatunzia lazima uwaandalie vizuri kwa
kuhakikisha huduma za msingi zinakuwepo na ni salama. Ili upokee vifaranga
lazma kama unapotaka kuwatunzia palishawahi kutumika uhakikishe panasafishwa
ili kuua wadudu/ visababishi vya magonjwa vinavyoweza kusababishwa au
kuambukizwa toka kwa wale waliokuwepo awali. lazima pasafishwe kwa dawa ili
kuuwa mabaki na kupafanya pawe salama. Pia inapendekezwa kabla ya kuwaingiza
hakikisha kwa chanzo cha joto ulichonacho unawawekea joto la kutosha kwano
vifaranga wanahitaji joto muda wote.
3. Joto, vifaranga wanahitaji joto muda mwingi hivyo
kulingana na uwezo na mazingira uliyonayo unapaswa kuwapatia joto kwani hata
wakiwa na mama yao muda mwingi wakiwa na baridi mama yao huwafuniaka na mbawa
zake ili wapate joto. Lengo la joto ni kumtengenezea kifaranga uwezo wa kuwa
timamu muda wote make akiwa na badiri kudorola na kudhoofika huwa vyepesi na
mwishowe hufa.
4. Ubora wa banda, malezi sahihi ya vifaranga yanahusisha
makazi sahihi ya vifaranga. Makazi ya banda lazima yamkinge kutokana na maadui
wa aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mazingira hasa baridi, wadudu kama
panya, utitiri, digidigi, na wengine wanaopatikana katika mazingira ya
mfuagaji, pia banda bora lazima liwe na miundombinu sahihi ya namna ya
kulisafishwa bila kuathiri maisha na ustawi wa hifaranga kwa mfano kwa kuwalelea
kwenye cages au hata banda lenye wavu kwa chi linalozuia vifaranga kula uchafu
na kinyesi chao nk.
5. Chanjo na madawa, kumekewa na wimbi kubwa la mahubiri ya
matumizi ya dawa za asili kwa ajili ya malezi ya vifaranga kitu ambacho ni
sahihi lakini bado tunakichukulia juu juu bila kinga ndani na kuangalia ukweli
na uhalali wake. Msisitizo wangu ni kwamba vifaranga wapate dawana chanjo
zilizopita kwenye maabara na sio zinazotolewa kwa kuhisia. Kama unataka kuwapa
miti shamba wape kama ziada kwani hakuna vithbitisho vya kitaalamu vya uwezo,
vipimo/viwango, ratiba na mambo mengine yote ya muhimu kwenye matumizi ya dawa.
6. Bluda, vifaranga inabidi waandaliwe sehemu yao ya
kuwalelea ambayo haina kona kwa maana vifaranga huwa wanakawaida ya kupenda
kukimbilia kwenye kona na kujirunda sehemu moja na mwishowe huwa wanauwana
lakini ukiwatengenezea bluda utaepuka hilo kwa maana bluda halina kona hivyo
kufanya vifaranga wasambae sawa maeneo yote. Pia bluda ni zuri kwa kuhihadhi
joto kwani huzuia upepo ambao ungeweza kuleta ubaridi kwani upepo huondoa joto
lililotengenezwa na kuleta hewa nyingine ya nje.
7. Chakula na maji, katika malezi ya vifaranga ni vizuri
kuzingatia chakula kinachoendana na vifaranga wako kwani kinakuwa na
mchanganyiko unaokidhi mahitaji ya vifaranga wako na pia texture yake itaendana
na vifaranga kwani zhakula cha vifaranga ni laini Zaidi. Pia chakula lazma
wapewe kwa kiwango stahiki maana sio unawapa kingi sana unaweza kusababisha
matatizo mengine kama chick pastig. Pia ikumbukwa kuwa mlo bora ndo nguzo ya
maishabora kwa vifaranga.
8. Usafi, hakikisha banda /bluda au eneo unalolelea
vifaranga wako ni safi ili kuepuka maradhi kwa maana Zaidi ya 75% ya magonjwa
ya kuku hutokana na uchafu na mlo hivyo hakikisha vifaranga wako wapo kwenye
eneo safi muda wote ili kuepuka kula chakula chenye kinyesi chao au kunywa maji
yenye kinyesi chao kwani huweza kusababisha magonjwa hatari kwa vifaranga kama
vile coccidiosisambayo huuwa sana vifaranga.
9. Uvumilivu wa vifaranga, pia kama mfugaji lazma ujue kuwa
uwezo wa kifaranga kuvumilia matatizo ni mdogo sana hivyo unalazimika kumjali
kwa kila mahitaji yake ya msingi na kumuongole hatari zote anazoweza kukutana
nazo kama vitu mumuangukia nk
10. Mwingiliano, vifaranga hawana uvumilivu na uwezo wao
kuimili magonjwa ni mdogo hivyo jiepusha na kuwachanganya vifaranga na kuku
wakubwa au unapotoka kutoa huduma kwa wakubwa badili mavazi esp viatu ili kama
kuna kibaya ulichotoka nacho huko kisiingie kwa wadogo. Pia pamoja na
muingiliano wa wafugaji wenyewe kutoka na kuingia kwenye mabanda yako kua sio
vizuri lakini pia nashauri vifaranga wasiwekwe kwenye maeneo ya karibu na kuku
wengine wakubwa kwani magonjwa mingine yanaambukizwa kwa hewa.
Kwa kuhitimisha ni kuwa idadi ya kuku watakaokuwa toka
kwenye vifaranga ni lazma itategemeana na idadi ya vifaranga vyako na matunzo
ulovipa. Usipovijali vifaranga hata idadi ya wakubwa pia usijali kwani
kinachotoka kinategemeana na ulichokiingiza.
0 comments:
Post a Comment