UKITAKA KUANZISHA MRADI WA KUKU ZINGATIA HAYA;
1. Malengo yako, je unahitaji wakue uwauze tu? unahitaji
kupata mayai na vifaranga kwa biashara? Iko hivi, kuku mzuri sana kwa nyma sio
mzuri sana katika utagaji na huo ni ukweli usiopingiga. Ukiona mtu anakuambia
anavyote at best level achana naye anakudanganya, Na si kwamba akiwa na nyama
hatagi no, sema utagaji wake sio mzuri kama wa wale wadogo wadogo na kinyume
chake.
2. Uwezo wako, nayo ni point ya msingi kwani usijeukafuga
wengi usioweza kuwatunza, nakushauri umpate mtaalam akuandalie bajet ili ujipime
kulingana na uwezo wako, ukikurupuka mara nyingi utaishia kujilaum.
3. Usimamizi wa mradi, lazma ujue huo mradi atausimamia
nani, wewe mwenyewe au mtu mwingine kwa niaba yajo. Inabidi ufanye maandalizi
ili uweke mpangilio utakaokupa wasaa mzuri wa kutekeleza majukum yako kama
utasimamia mwenyewe, ikiwa ni pamoja na kutafuta utaalam kwanza kabla
hujaingiza vifaranga. Kama utamtumia mtu lazma naye umtafutie utaalam ili awe
na walau basic knowledge kwa ajili ya kulea mradi. ukibeba beba tu mtu na kumpa
afanye unaweza kulia ndani ya wiki wakafa wote.
4. Mazingira utakayofugia, hapa zingatia usalama wa kuibiwa,
wadudu, wanyama, magonjwa ya kuenezwa, muingiliano nk.
5. Soko linataka nini, fuga kitu kitakupa uhakika wa
biashara lakini epuka kabisa biashara za msimu/ biashara za kuzuka. Ukijiingiza
kwenye biashara hizo mara nyingi huwa zinakuwa na ukomo/ kuisha fasheni.
ukiingia kwenye kufuga kwa fasheni maana yake unaweza ingiza gharama zako na
saa ya kuvuna ukajikuta soko la bidha zako lishaisha au kuwa dogo..
0 comments:
Post a Comment