MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE
Kuku kama wanyama wengine hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ambayo huzuia magonjwa hayo.Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku.
A.) MAGONJWA YANAYOHITAJI CHANJO
1> GUMBORO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
DALILI ZA UGONJWA
-Kuku kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
-Kuku kuharisha
-Kuwa na vifo vingi kwa kuku
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za
oxytetracycline hupunguza vifo.
KINGA
wakinge kuku wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro
vaccine)
2> MAHEPE (Marecks)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi
DALILI
-Kuku hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba
KINGA
Chanjo hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa siku
moja,vifaranga hupewa chanjo ya mahepe (Marecks vaccine)
3>NDUI YA KUKU (Fowl Pox)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
DALILI
-Kuku hupatwa na vidonda kichwani.
-Kuku hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba.
KINGA
Chanja kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku
(Fowl pox vaccine).
4>MDONDO (New castle)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi
DALILI
-Ugonjwa huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
-Vifo vya kuku huwa vingi
-kuku hupumua kwa shida
-Kuku hupooza na kulemaa miguu
-Kuku hupinda shingo yake
-Kuku hupunguza kutaga mayai
-kuku huarisha
-Kuku Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.
TIBA
Hauna tiba
KINGA
Chanja vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New
castle vaccine) na urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.
B.)MAGONJWA YANAYOTIBIKA KWA DAWA
1>KUHARA DAMU (coccidiosis)(Koksidiosisi
Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
DALILI
-Kuku huzubaa na kujikunyata
-Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia
-Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na
kuonekana kama wawevaa koti
-Kuku hupungukiwa homa ya kula
-Vifo huwa vingi kwa vifaranga
TIBA
Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.
KINGA
Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu
katika banda la kuku,
2>HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
Husababishwa na bakteria
DALILI
-Kuku hupata homa kali
-Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
-Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
-Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa
hamu ya kula
TIBA
Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu
ugonjwa huu.
KINGA
Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa
kuku.
Tenganisha kuku wagonjwa na wazima
C)MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga
DALILI
-Kuku hukonda
-Kuku huarisha
-Kuku hukohoa
-Kuku hupunguza utagaji
-Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
-Kuku hupungua uzito
TIBA
Tumia dawa za minyoo kama piperazine
KINGA
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi
mitatu
D)VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa
vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa
sana.
DALILI
-Kuku kutochangamka
-Ukuaji mdogo wa kuku
-Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa
na chawa,utitiri au viroboto
-Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu
TIBA
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri
powder kwa kuku wote na mabanda yao.
KINGA
Boresha usafi wa mabanda ya kuku.
E)UKOSEFU WA VITAMINI A
huathiri sana kuku wadogo.
DALILI
-Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya
kipande iliyolowana.
-Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha
kiangazi
TIBA
wape kuku wote dawa za vitam
0 comments:
Post a Comment