Our social:

Friday, December 16, 2016

KWANINI KUKU WAKO HAWATAGI UNAVYOTAKA?


Image result for EGGYS TRAYS

1. ULIKOSEA KUCHAGUA AINA . kuku wapo aina nyingi sana na kila mmoja na sifa yake, 
unashauriwa kabla hujachagua aina ya kuku unayoitaka kuifuga ujiridhishe kama itakupa unachokihitaji, mfano ukitaka ya mayai mengi lazma uchague anayetaga sana na ukitaka mwenye nyama nyingi lazma uchague mwenye nyama nyingi. Mainly kwa kuku tulionao na tunaowafugwa kwa milady ya kuku hapa nchini kitaalamu ni wa aina mbili, standard bleed na high bleed. Kila mmoja na uzuri wake na ubaya wake.

2. HAUWAPI LISHE INAYOSTAHILI, ukiwa mfugaji lazma ujue matakwa ya mifugo yako kwa wakati husika, kuku anayekua anahitaji chakula chakumkuza na kumuhimalisha, vifaranga wanahitaji chakula laini kwa ajili ya mmengenyo na protin ili kutengeneza joto la mwili, hivyo hivyo na kuku wanaotaga ao wanahitaji chakula kwa ajili ya kutengeneza mayai kwa wingi kwa maana chakula kiwe na content muhimu.
Image result for black australorp hen
3. MAZINGIRA UNAYOWAFUGIA, ili kuku aweze kutaga vizuri lazma umuwekee mazingira rafiki kwa ajili ya hilo suala, mazingira yenye usafi na umtengenezee viota kwa ajili ya kujistili. Kaa ukijua suala la kutaga kuku au hata ndege wengine wengi kwao ni suala la siri hivyo ili liweze kufanyika kwa ufasaha na kuku ashawishike kutaga lazma umuwekee kauficho ambapo akiingia atamaliza haja zake. Kuku wanaweza kutimiza umri wa kutaga lakini wasitage kama hujawatengenezea mazingira rafiki kwa ajili ya hilo jambo.

4. MAGONJWA NA WADUDU, sifa kuu ya ugonjwa ni pamoja na kuudhoofisha mwili na kitendo cho kudhoofu kwa mwili lazma kitaathili utengenezekaji wa mayai mwilini mwake hivyo ili uweze kuvuna vizuri inabidi ujitahidi kuwa kuku wako wana afya bora hawasumbuliwi na maradhi. Pia suala la wadudu mithili ya utitiri nk ni wabaya sana kwa kuku watagaji kwa maana ili kuku atengeneze yai na atage inabidi awe katika sehemu tulivu, sasa kama anasumbuliwa na wadudu hata kutaga lazma kuathiliwe moja kwa moja.

5. RATIBA YA CHAKULA, ili kuku awe na ufanisi lazma awe na trend inayoelewekwa, kwamba muda flani ni wake kula na muda flani ni wa kutengeneza yai. Ukimbadirishia kuku ratiba ya chakula lazma utagaji utaathirika mpaka azoee na kama ndo kila siku unambadirishia huzingatii muda wa kumpa chakula basi utegemee utagaji hafifu. Pia kuku sio kwa kuwa unahitaji mayai basi ndo unampa chakula kingi ndo atage sana, no, ukimshindisha anakula asubuhi mpaka jioni ataishia kukufilisi na mayai hatotaga au atataga kigogo sana, kuku chakula inabidi umpe kwa viimo na wakati, akimaliza chakula basi.

6. UTULIVU WA AKILI NA MWILI, hii pia ni sababu kubwa kwamba ili kuku atage vizuri lazma awe na utulivu kiakili na kimwili, mfano, hata kama kuku alikuwa anataga ukimtoa kwenye mazingira yake ya awali na kumsafirisha kwenye maeneo mengine lazma kwanza atakaa kwa muda mpaka azoee hali, mfano unamtoa kuku tabora unampeleka Zanzibar, possibly efficiency yake katika utagaji itapungua kwa kipindi ambacho hajazoea mazingira na hali ya hewa. Hata ukimtoa kwenye cage na kumuweka chini au kumtoa chini kwenye banda la kutumia viota na kumuweka kwenye cage, lazma atumie muda kuzoea hivyo inaweza athiri utagaji.


7. MZUNGUKO WA MWILI, kikawaida kuku huwa wana muda wa mapumziko ya kutaga, kuna kipindi ikifika kuku huwa wanastop au kupunguza kutaga kwa maana huwa wanakuwa ni kama wamechoka au wameishiwa hivyo wanajiunda upya. Hili hasa hutokea baada ya kipindi kilefu cha utagaji hivyo kama ufugaji lazma ujue kuwa hii ni hali ya kawaida na ndo likizo zao pia make hata binadamu ikifikwa muda baada ya kazi ngumu huwa tunajipa rikizo.

0 comments:

Post a Comment